}

AZAM YAENDELEA KUJIFUA ILI KUIUA RUVU SHOOTING WIKIEND HII

Picha na Anaseli S,Macha
Uongozi wa klabu ya Azam FC,umesema kwamba kikosi chao kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Afisa Habari wa Timu hiyo,Jafari Idd amesema kwamba kwa upande wao wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanachomoza na ushindi katika mchezo huo unaotaraji kupigwa kwenye uwanja wa Azam Complex siku ya jumamosi kuanzia saa moja usiku.

Jafari anamini kuwa mchezo huo utakuwa ni mgumu kwa kila timu lakini nguvu zote kwa sasa wamezielekeza katika mchezo huo ili kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu.


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.