}

MAYANGA; MKUDE NA MUDATHIR WAONGEZWA KIKOSINI

Kocha wa timu ya Taifa Tanzania Salum Mayanga amefanya mabadiliko katika kikosi chake kwa kuwaita wachezaji kiungo wa klabu ya wekundu wa msimbazi simba Jonas Mkude na Mudathir Yahya baada ya  kupata ufafanuzi juu ya wachezaji Erasto Nyoni na Mzamiru Yasin ambao katika mchezo dhidi ya malawi walipata kadi nyekundu.

Mayanga amelezimika kufanya mabadiliko hayo ili kukipa nguvu kikosi hicho kutokana na kutokuwepo kwa wachezaji hao muhimu kungeweza kuleta pengo katika kikosi chake ambacho kinatarajia kuelekea Benin kwa ajili ya mchezo wakirafiki ulio katika kalenda ya FIFA.

Kikosi cha timu ya taifa kinatarajiwa kuingia kambini manamo tarehe Tano kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo dhidi ya Benin mchezo unaotarajiwa kupigwa tarehe 12 mwezi huo huku nchini Benin.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.