Naibu waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh. Faustine Ndungulile ameitaka mamlaka ya chakula na dawa TFDA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa
Naibu waziri wa Afya maendeleo
ya jamii jinsia wazee na watoto Mh. Faustine Ndungulile ameitaka mamlaka ya
chakula na dawa TFDA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ili dawa zote
zinazoingia nchini ziwe na ubora unaohitajika
Mh. Ndungulile amesema hayo
jijini dar es salaam katika uzinduzi wa Cheti cha mfumo wa uhakiki ubora wa
huduma cha kiwango cha kimataifa cha ISO ambapo amesema kuwa kupatika ka Cheti
hicho ni wazi kuwa mchango wa mamlaka ya chakula na dawa TFDA ni mkubwa kwa
taifa hivyo wanatakiwa kuongeza juhudi ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Kwa upande wake mkurugenzi
mkuu wa TFDA Bw.Hiiti Sillo amesema tangu walipopata Cheti hicho wamefanya ukaguzi
wa kila mwaka ili kubaini kama bado mfumo huo unakidhi matakwa ya kiwango cha
kimataifa na kusisitiza kuwa mfumo huo umezidi kuimarika na kutoa huduma sahihi
kwa watumiaji.
No comments