}

MKURUGENZI SMILE STARS ATTORNEYS AWATAKA WATANZANIA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI.

Na. Happy Shirima-Dar

 Mkurugenzi mtendaji wa smile Stars attorneys Leonard Manyama amempongeza raisi wa jamhuri ya muungano ya Tanzania John magufuli kwa jitihada zake za kupambana na rushwa na ufisadi, ujangili, madawa ya kulevya pamoja na wizi wa rasilimali za nchi ikiwemo madini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam bw. Manyama amesemakuwa jitihada hizo zimesaidia kupotea kwa pesa zilizokuwa zinapatikana kwa njia haramu na kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya serekali kila mwezi kutoka bilioni 800 mwaka 2015 hadi trillion 1.2 kwa mwaka 2017.

Aidha ameongeza kuwa madhara ya fedha haramu ni pamoja na wanyonge na maskini kukosa haki, uvunjifu wa sheria pamoja na kuathiri mifumo ya siasa na uchumi wa nchi.

Hata hivyo ameongeza kuwa watanzania washirikiane kwa pamoja katika kipindi hiki cha kupanda ambapo wakati utafika na watakula matunda ya uwekezaji unaofanywa na raisi pamoja na serekali yake.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.