}

MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO AWAOMBEA ARDHI YA KILIMO KWA MAGEREZA VIJANA WATAKAOKOSA NAFASI ZA JKT.


Na. Anaseli Stanley Macha.

Mkuu wa wilaya ya bagamoyo kwa kushirikiana na kamati ya ulinz na usalama wilayani humo leo wameendesha zoezi la usaili wa kuwapata vijana 65 watakaoenda katka ngaz ya mkoa kusaka nafasi ya kujiunga na jkt ambapo zoez hilo linatarajiwa kumalizika hapo kesho.

Akizungumza na vijana zaidi ya 1170 ambao wamejitokeza kuomba nafasi ya kujiunga na jkt mh majid amesema nafasi za kujiunga na jeshi hilo ni chache ukilinganisha na wingi wa vijana hao hvyo ni vyema wale watakakosa waungane kwa pamoja ili kulima kilmo cha mihogo viazi na mazao mengne mbalimbali.

Kufuatia kauli hivyo mkuu wa wilaya amemwomba mkuu a gereza la kigongon wilayan humo hekari 50 za shamba kwa ajili ya vijana watakao kosa kuchaguliwa kujiunga na jesh la kujenga taifa jkt ili kujihusha na kilomo.

Kwa upande wake mkuu wa gereza la kigongoni kamanda mihengi amekubali kutoa eneo hilo kwa mkuu wa wilaya ya bagamoyo kwa ajili ya vijana 1105 ambao watatoka katika mchujo wa vijana 1170 ya walioomba nafasi ya kujiunga na jkt wilayan humo.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.