}

MAKAMPUNI YA BIASHARA YATAKIWA KUZINGATIA HAKI ZA BINADAMU.

Na. Happy Shirima-Dar.


MAKAMPUNI  ya  kibiashara nchini yametakiwa kuzingatia haki za binadamu zilizoainishwa kisheria ikiwemo Ajira,Mazingira na usalama kazini ili kuepusha malalamiko yanayokua yakiripotiwa mara kwa mara kutoka kwa wananchi.

Mapema Leo hii, akizunguza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume ya haki za binaadam na utawala bora Bahame Nyanduga wakati akizindua mpango wa uchunguzi wa taratibu wa haki za binaadam kwenye biashara ulioandaliwa na tume hiyo pamoja na asasi za kimataifa.

Amesema kuwa mpango huo utasaidia na kuangalia namna makampuni yanaweza kufanya kazi katika kufuata misingi ya haki za kibinaadam ambazo wamekubaliana katika nchi wanachama wa umoja wa mataifa katika kutekeleza malengo endelevu ya kimaendeleo.

Aidha ameongeza kuwa, endapo mpango huo utakamilika Tanzania itakua ni nchi ya kwanza barani Afrika kuweza kusimamia na kutekeleza haki za binaadam katika makampuni ya kibiashara.

Katika hatua nyengine Afisa Uchunguzi mwandamizi  (CHRAGG) Jovina Muchunguzi amesema kuwa, ukiukwaji  wa haki za kibinaadam unatokea sana katika makampuni mbali mbali ikiwemo yale ya uchimbaji wa madini , kilimo,biashara  pamoja na utalii.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.