}

SERIKALI YADHAMILIA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WATOTO.

Na. Happy Shirima-Dar.


SERIKALI kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeandaa mpango kazi wa taifa katika kutokomeza ukatili dhidi ya mtoto kwa kupunguza mimba na ndoa za utotoni kwa asilimia 27.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ,Mkurugenzi wa maendeleo ya watoto kutoka wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Margaret Mussai katika kongamano la watoto wakike lililoandaliwa na jukwaa la utu wa mtoto (CDF).


Amesema kua,Serikali imekua ikifanya juhudi mbalimbali katika,kutimiza lengo lake la kielimu pamoja na kukabiliana na changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni na mimba za utotoni.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa shirika hiyo, Consuma Mtengei amesema kuwa ,lengo la kongamano hilo ni kuwapatia fursa watoto wa kike katika utekelezaji wa miradi inayofanywa na shirika hilo ikiwa ni pamoja na kutokomeza ukeketaji,mimba na ndoa za utotoni.

Aidha ameongeza kuwa, shika la CDF limekuwa likiwasaidia watoto wa kike waliofanyiwa ukatili wa kijinsia kwa kuwapatia mafunzo ya ujasiri amali ili

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.