}

LUCAS; KILIMANJARO HEROUS IMEANDALIWA KUPAMBANA CHALLENGE NCHINI KENYA

Kikosi cha timu ya Taifa Tanzania bara Kilimanjaro Herous kimeendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya CECAFA Challenge Cup ambapo kilimanjaro herous itafungua desemba 3 dhidi ya libya.

akizungumza na na Kituo cha habari Blog Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania Afred lucas amesema kuwa wachezaji wote wamewasili kambini isipokuwa kiungo wa Azam Himidi Mao Mkami ambaye huenda akaenda Africa Kusini Kwa ajili ya kufanya majaribio na moja ya klabu nchini humo.

lucas pia amethibitisha kikosi hicho huenda kikakosa mchezo wa kujipima nguvu kabla ya kuingia katika michuano hiyo kutokana na mikakati ambayo ilipangwa kutoenda sawa.

Wakati wowote kikosi hicho kinatarajia kukwea pipa kuanza safari ya kwenda nchini kenya kushiriki michuano ya Cecafa Challenge Cup.


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.