}

KUAPISHWA KWA KENYATA, RAIS MAGUFULI AMTUMA MAMA SAMIAH KUMUWAKILISHA.

Na.Anaseli Stanley Macha.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu imesema Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na kupokelewa na Balozi Robinson Njeru Githae wa Kenya na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Pindi Chana.

Sherehe za kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta zimefanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi Nchini Kenya.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.