}

AZAM FC YASAHAU MATOKEO YAO NA MTIBWA YAJIPANGA MICHUANO YA MAPINDUZI CUP.

Na.Anaseli Stanley Macha.

Klabu ya  Azam imethibitisha kushiriki michuano ya mapinduzi ambapo imepanga kuhakikisha inaenda kutetea Taji la mapinduzi cup kutokana na umuhimu wa michezo hiyo katika kuimarisha kikosi chao kama sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara.
Afisa habari wa klabu hiyo Jafari Idd Maganga amesema mwalimu atapeleka kikosi chote ili kuhakikisha wanaleta ushindani kama msimu uliopita wa michuano hiyo.

Ingawa katika mwaka uliopita Azam haikupewa nafasi ya kutwaaa kikombe hiko Jafari amesema watawasili Zanzibar mapema ili kupata nafasi ya kufanya mazoezi ya kujiandaa na michuano hiyo ambapo wanaamini itawapa fursa vijana na mwalimu kupanga na kuenda sawa na ratiba ya mazoezi ya kuijianadaa na michuano hiyo.
Azam imepangwa na klabu ya wekundu wa msimbazi simba na timu nyingine za unguja Jafari anaamnini kuwa kundi hilo litakuwa gumu kwani timu zote zimejiaandaa vyema.

Baada ya Azam kumaliza mchezo wao wa 11 na klabu ya Mtibwa Sukari  na kila mmoja kuambulia alama moja uongzoi wa azam umesema wanawashukuru benchi la ufundi na wachezaji waote kwa namna walivyopambana kuhakikisha hawakupoteza mchezo huo.
Goli la kuongoza la Azam Fc lilifungwa dakika ya 56 ya mchezo na Agyei timu hiyo ilipocheza na Mtibwa Sugar ambao walichomoa goli hilo na matokeo kubaki moja moja.
Jafari Idd Maganga amesema mchezo huo ulikuwa ni mgumu kwa pande zote mbili lakini haikuwa rahisi kwao kupata ushindi ila walichokipata wanaridhika nacho.
Azam juzi ilikipiga dhidi ya Mtibwa Sukari ya kule Manungu ambapo katika mchezo huo ulimalizika kwa kila timu kupata bao moja na alama moja .

Baada ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la Usajili Klabu ya Azam imesema imefunga usajili kwa kumsajili mchezaji raia wa Ghana Bernad Artha na hakuna mchezaji mwingine yeyote ambaye atasajiliwa katika klabu hiyo
Jafari Iddi Maganga amsema walikuwa na tatizo katika eneo la ushambuliaji lakini wanaamini baada ya kumpata mshambuliaji huyo eneo hilo litakuwa vizuri kwa hivi sasa.

Hivi karibuni klabu hiyo ilimfungia vilago mshambuliaji wao Yahaya Mohamed sasa Artha anakamilisha usajili wao na kuziba nafasi ambayo imeachwa na mshambuliaji huyo.
Jafari amesema kocha hana mpango wa kuacha wachezaji mwingine yeyote na hata kuongeza mchezaji mwingine na wachezaji waliopo ndio watakao maliza katika michezo yote iliyobaki aidha ya ligi na mingineyo.

Kiungo na kapteni wa klabu ya azam Himid Mau Mkami amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi ocktoba baada ya mashabiki wa klabu hiyo kumchagua mchezaji hiyo
Mau amewashinda wachezaji wenzake wengine na uongozi wa klabu hiyo umempongeza kwa kiwango alicho kionesha katika michezo yote ya mwezi octoba.

Klabu ya azam imekuwa na utaratibu wa kuwapa fursa mashabiki wao kumchagua mchezaji bora wa mwezi kwa kumpigiz kura katika mitandao ya kijamii.



No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.