}

MASHINDANO YA MABUNGE KUANZA KUTIMUA VUMBI DESEMBA 1.

Na.Mussa Omary Said.


Mashindano ya mabunge Ya  Afrika Mashariki yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia desemba 1 had 11 mwaka huu katika viwanja vya taifa jijini dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa bunge sports club William Ngeleja, Amesema maandaliz ya mashindano hayo yamekamilika.

Ngeleja amesema mashindano haya yatahusisha michezo ya soka, pete wavu kwa wanaume na wanawake gofu wanaume na wanawake kuvuta kamba,riadha na kutembea kwa mwendo kasi.

Aidha amezitaja timu za mabunge ya nchi za jumuiya ya Afrika mashariki ambazo zitashiriki kuwa ni Tanzania, Kenya, Uganda, Birundi Ruwanda na Sudan Kusin na timu ya bunge la nchi za  jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katika hatua nyingine Ngeleja ameizungumzia timu ya bunge la Tanzania kwamba imeendelea kufany mazoez katika viwanja vya jk park kwa lengo la kujiimarish kichukua ubingwa wa mashindano hayo.

Pamoja na hayo Ngeleja amewatak watanzania hususan wakaz wa jiji la dar es salaam na mikoa ya jirani kujitokeza kushuhudia vipaji vy michezo walivyonavy waheshimiw wabunge na watumishi wa taasis za bunge.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.