}

LWANDAMINA AWAPA WIKI NYOTA WAKE KUPUMZIKA

Kikosi cha Yanga sasa kinatarajia kuwa na mapumziko ya siku kadhaa baada ya  Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina kutoa ruhusa kwa nyota wake kupumzika kwa  wiki  moja.

Baada ya ya ligi kuu kusimama kupisha michuano ya CECAFA CHALLENG CUP Kikosi cha Yanga kipo mapumziko baada ya kucheza mechi 11 na kikiwa katika  nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam katika Ligi Kuu Bara huku mchezo wa mwisho timu hiyo ikiwa imecheza dhidi ya Tanzania Prisons na mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Yanga ina pointi 21, ikizidiwa pointi mbili mbili na Simba, sawa na Azam FC ambayo jana ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.