}

KILIMANJARO STARS TUTARUDI NA UBINGWA WA CHALENJI CUP


Na. Anaseli Stanley Macha.

Kocha wa kilimanjaro stars Ammy Ninje amewatakata watanzania kutoa ushirikiano mkubwa wakati timu hiyo itakapokuwa katika mshike mshike wa michuano ya chalenji Nchini Kenya ili kutimiza lengo la kurudio na ubingwa wa michuano hiyo.

Kocha Ninje amesema hayo wakati timu hiyo ikiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini kenya kwa ajili ya michuano ya chalenji ambapo Kilimanjaro Stars itatupa karata yake ya kwanza kukipiga dhidi ya Libya siku ya jumapili.

Ninje amesema kikosi chake kipo vizuri hakuna aliyemajeruhi na wachezaji wote wana hali ya kupambana kwa ajili ya Taifa lao.

amesema kila kitu kinawezakana kwani anawachezaji wengi ambao wanampa fursa ya kufanya mabadiliko mengi ya kimfumo katika michezo yake ambayo anaamini atapata matokeo mazuri katika kila mchezo.

Aidha amesema hana sababu ya kuwaangalia zaidi wapinzani wake lakini anaamini amekiandaaa vyema kikosi chake kupambana na kila atakae kuja mbele yake.


Nae golikipa wa timu hiyo Aishi Manura amesema wamejiandaa vyema na wanaamini watayatumia vyema maelekezo ambayo kocha  Ninje ameyatoa kwao.

Manura piaamewataka watanzania kuwa na imani na timu yao kwamba itarudi na kombe la michuano hiyo.





No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.