}

GHARAMA ZA USAJILI WA VYAMA VYA MICHEZO ZAPANDA

Kulia ni waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Dkt.Harrison Mwakyembe , katikati ni mkurugenzi wa michezo wizara ya habari utamaduni sanaa na michezo Yusuph Singo  na Mwisho  ni Msajili wa vyama vya michezo bw. Ibrahim Sapi Mkwawa.
Msajili wa vyama vya michezo kupitia kitengo cha Habari cha baraza la michezo Tanzania BMT,Ibrahim Sapi Mkwawa leo hii ametangaza rasmi mabadiliko ya ada mbalimbali ya usajili wa vyama na vilabu vya michezo.

Mkwawa amesema mabadiliko hayo yamefanyika kwa mujibu wa kanuni ya 25 fasili ya 5 ya kanuni usajili wa vyama vya michezo . 

Amesema Ada kwa vyama vya micheo vilikuwa vimegawanyika katika sehemu kuu tano ambapo kuna vyama vya kitaifa mfano Tff ,Chaneta au chama cha Riadha,  lakini pia kuna vyama vya mikoa, wilaya, vilabu,na  wakuzaji na mawakala wa michezo ambapo gharama za ada zote zilikuwa katika kiwango kidogo ambazo hulipwa kwa mwaka.

Aidha Mkwawa amesema baada ya kupitia upya na kufanya Tathimini wamepitisha  gharama mpya ambazo kila chama kitakapohitaji kufanya usajili kitapshwa kulipa gharama kama ifuatavyo...

1. Vyama vya kitaifa mfano Tff ,Chaneta au chama cha Riadha, wao watalipa  sh.100,000. ambapo zamani hawa walikuwa wanalipa  sh.25000.

2. Vyama vya Mkoa nao watalipa sh.50,000. badala ya sh. 20,000.

3. Vyama vya wilaya watalipa sh. 25,000

4. Vilabu vilatalipa sh. 20,000

5.Vituo vya michezo pamoja na Academy viltalipa sh. 100,000

6. Wakuzaji na mawakala  sh. 100,000.

7.  Cheti cha usajili kitatozwa sh. 20,000.

8 .Maombi ya kukagua register ya msajili yatatozwa sh.20,000.

9. Maombi ya kivuli cha cheti ambacho kimepotea ni Sh. 20,000.

10.  Maombi ya hati iliyothibitioshwa na Msajili  nayo itakuwa sh. 20,000.

Na maombi mengineyo yote yatatozwa sh. 20,000.





No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.