}

UMOJA WA MATAIFA WAITAKA KONGO KUHESHIMU UHURU WA KUANDAMANA.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umewataka maafisa nchini humo kuheshimu uhuru wa kuandamana wakati ambapo leo vyama vya upinzani vimeitisha maandamano ya umma ambayo serikali imeyapiga marufuku.

Upinzani unaoongozwa na Felix Tshisekedi umeapa utaendelea na maandamano hayo kuupinga utawala wa Rais Joseph Kabila ambaye alipaswa kuondoka madarakani mwezi Desemba mwaka jana baada ya muhula wake wa pili kumalizika. Nini hatima ya Kongo? Ndio swali linaloendelea kubakia miongoni mwetu.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.