}

Ajali barabarani zalitesa jeshi la Poli Dar.


Jeshi la polisi la usalama barabarani kanda maalum mkoani Dar es Salaam wanakabiriwa na changamoto ya ajali mbalimbali za barabarani zinazosababishwa na vyombo vya moto. 

Akizungumza na waandishi wa habari. Kamanda mwandamizi wa jeshi la polisi Fotinatus Musilim, akitakitoa taarifa ya maandalizi ya wiki ya nenda kwa kusalama barabarani itakayoanza tarehe 18-26 November mwaka huu mkoani kinondoni  wakifadhiliwa na benki ya starnbic, amesema kuwa jeshi la polisi wakishirikiana na benki hiyo wamejioanga kupunguza ajali barabarani kwa kutoa elimu juu ya matumizi barabara na alama zake ili  kupunguza vifo vya watu kwa makosa ya madeva wasiotii sheria na pia amesistiza zoezi la kukamata halitoisha kwa madereva wazembe na kwamwe hawatabaki salama kwa kasi hiyohiyo .

Nae  mkuu wa matawi ya benki ya  Stanbic amesemakua wako pamoja na jeshi la polisi  kushirikiana kuhakikisha ajali zinapungua ama zinaisha kabisa.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.