}

Ajali yaua 8 kujeruhi 12 katika tukio la kigaidi.

Gari iliyogonga na kusababisha vifo na majeruhi mjini New York.
Watu 8 wamefariki Dunia na wengine 12 kujeruhiwa baada ya gari kuwagonga watembea kwa miguu mjini Newyork. 
Meya wa mji wa New York, Bill De Blasio, amelielezea tukio hilo kuwa la ugaidi lililosababisha hofu mjini humo.
Kamishna wa polisi wa jiji wa New York, James O'Neill, amemuelezea mtu aliyewtekeleza tukio hilo kuwa ni kijana wa miaka 29 aliyekuwa anaendesha gari ndogo la kubebea mizigo alilokuwa amelikodi.
Alisema gari hilo liliwagonga watembea kwa miguu na wapanda baiskeli kabla ya kugongana na basi la shule.
Kwa upande wake bwana O'Neill, amesema kuwa dereva wa gari hilo alitoka ndani ya gari lake na kuanza kuandaa silaha mbili kwa ajili ya shambulizi na kabla ya hilo, polisi walimuwahi na kumpiga risasi zilizomjeruhii.
Polisi mjini humo wametoa tamko kwamba wanalichukulia tukio hilo kama shambulizi la kigaidi , Mtuhumiwa wa tukio hilo alichukuliwa na polisi kwa mahojiano zaidi ambao walithibitisha taarifa hizo katika kituo cha Lower Manhattan.
Vyombo vya habari nchini Marekani vimenukuu taarifa za polisi kuwa kijana huyo aliamua kuendesha gari hilo katika njia ya waendesha baisikeli iliyoko karibu na Mto Hudson eneo la Lower Manhattan ya chini ,kabla ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi ili kuzuia shambulio alilolipanga.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.