}

YANGA MAZOEZI YANAENDELEA KUWAKOSA NGOMA TAMBWE NA KAMUSOKO

KIKOSI  cha Yanga leo kimeanza mazoezi ya uwanjani kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Singida United mchezo utakaopigwa siku ya jumamosi katika Uwanja wa Namfua Mkoani Singida.
 
Akizungumza maandalizi hayo, Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema maandalizi ya kikosi hicho kwa ajili ya mchezo dhidi ya Singida yanakwenda vizuri katika kuhakikisha wanapata pointi tatu muhimu.

Katika mazoezi hayo,  wachezaji  Amissi Tambwe na Wazimbabwe, Thabani Kamusoko na Donald Ngoma hawakuonekana kutokana na kuendelea kuwa majeruhi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.