}

MANARA;WAAMUZI WANAENDELEZA DHURUMA KUIHUJUMU SIMBA

KLABU ya Simba imetoa malalamiko yao juu ya waamuzi kutokana na  kunyimwa penalti mbili na refa Heri Sasii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC uliomalizika kwa sare ya 1-1 Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari,  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Sunday Manara amesema waamuzi wa wanaochezesha Ligi kuu tanzania  Bara wamekuwa na mtirirko wa kutoa maamuzi mabovu katika michezo yao na huenda wanapokwenda uwanjani wanakuwa na matokeo yao.




Manara aliwawekea Waandishi wa Habari video ya mchezo michezo mitatu ule wa mbao, stend United, na  wa watani wao Yanga kuonyesha namna ambayo waamuzi katika michezo hiyo walivyokuwa na maamuzi mabaya kwa klabu yao 

Manara amewaeleza wanandishi wa habari na  kuwaonyesha namna ambavyo refa Sasii hakutoa penalti katika mchezo wao na watani wao licha ya mpira kuwagonga mikononi beki, Kevin Yondan na kiungo Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi Jumamosi.


Aidha Uongozi wa klabu ya Simba umeliandikia barua shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF kueleza malalamiko yao dhidi ya waamuzi

Manara  amethibitisha kuwaandikia Barua TFF pamoja na bodi ya ligi huku pia nakala wakiiwasilisha kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ili watambue malalamiko yao.

katika michezo yao mitatu  waamuzi hao wameshindwa kutafasiri vyema sheria 17 za soka hasa katika mechi zao  dhidi ya Mbao FC,Stend United pamoja na mahasimu wao wa jadi Yanga.

Alisema kwamba katika mechi hizo waamuzi walionyesha dhuluma ya wazi kwa klabu ya Simba kwani maamuzi yaliyotolewa yalikuwa ni ya utata pamoja na kuwanyima penati ambazo zilikuwa za waz


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.