}

Uhuru Kenyatta ashinda Urais nchini Kenya.

Ukumbi maalum ulioandaliwa na tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC kwaajili yakumtangaza mshindi wa Uchaguzi wa marudio.

Uhuru Kenyatta ndiye rais mteule wa taifa la Kenya baada ya kuzoa kura milioni 7.4 ya kura zote zilizopigwa kwenye uchaguzi mpya wa urais, ametangaza mwenyekiti wa tume ya IEBC, Wafula Chebukati.

Uchaguzi wa marudio wa Kenya ulifanyika tar.26 oktoba mwaka huu baada ya Mahakama ya nchi hiyo kutengua matokeo ya awali ya Uchaguzi mkuu.

Kiongozi mkuu wa Upinzani kupitia umoja wa vyama vya upinzani NASA amesusia Uchaguzi huo na kushinikiza wanachama wake kutokwenda kupiga kura.

Chanzo-DW

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.