}

Lazaro Nyalandu ajivua Ubunge nakuihama CCM.

NA. Geofrey Jacka.

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu.

Nchini Tanzania mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu amejiuzulu kutoka chama tawala cha CCM.

 Nyalandu aliyekuwa Waziri wa Maliasili wa taifa hilo ameelezea kutoridhishwa kwake na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini humo pamoja na ukiukwaji wa haki za binaadamu, ongezeko la vitendo vya dhulma wanavyofanyiwa baadhi ya Watanzania.

Nyalandu amekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini kwa miula minne tangu mwaka 2000 na amefikia maamuzi hayo leo hii huku akiweka nia yake yakujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.