}

Serikali yadhamiria kutokomeza Uvuvi haramu.

Na. Happy Shirima.

Wananchi wakitazama zoezi la uchomaji moto nyavu na vifaa vya uvuvi haramu wa Samaki. (Picha. Maktaba).

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeadhimia kukomesha uvuvi haramu hapa nchini,ili kuweza kuhakikisha samaki wanazalishwa kwenye mazingira mazuri na yenye ubora.

Hayo yamejiri jijini Dar es salaam katika ufunguzi wa mkutano wa siku 6 uliowakutanisha wadau wote wa bahari ya Hindi,unaojadili kuhusiana na uhifadhi na utunzaji endelevu kwa ajili ya viumbe hai vilivyomo kwenye bahari hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN Waziri wa Mifumo na Uvuvi LUHAGA MPINA amesema kuwa Serikali haiwezi kuzungumzia suala la uvuvi haramu bila kufikia mwisho hivyo ni lazima kuhakikisha uchafuzi unaofanyika baharini unafikia kikomo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo Prof YUNUS MGAYA amesema kuwa nchi ya Tanzania inakabiliwa na changamoto ya ongezeko la joto Hali inayopelekea kufa kwa matumbawe pamoja na kupoteza rangi yake ya asili.

Aidha amesema mkutano huo utatoka na marekebisho ya sera na Sheria mbalimbali zinazosimamia viumbe hai wa baharini,hali itakayopelekea kulinda rasiliamali za nchi za ukanda wa Afrika.

Ameongeza kuwa licha ya kuwepo kwa ongezeko la fursa za utumiaji wa leseni ni vyema wavuvi wakavua samaki kwenye kila kirefu cha maji ambayo yanasimamiwa na chombo cha Muungano wa Serikali ya Tanzania na Zanzibar.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.