}

Tutaendelea kutengeneza Makombora-Iran.


Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema leo kwamba Iran itaendelea kutengeneza makombora kwa ajili ya ulinzi wa nchi yake na hailizingatii hilo kama ukiukaji wa sheria za kimataifa. 


Rouhani ameyasema hayo siku chache baada ya Baraza la Wawakilishi la Marekani kupiga kura ya kuuwekea vikwazo vipya mpango wa makombora wa Iran, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuishinikiza Iran kabla ya kuyadhoofisha kabisa makubaliano ya kimataifa kuhusu silaha za kinyuklia kati ya Iran na nchi nyingine kadhaa. 

Rouhani ameongeza kwamba wataendelea kutengeneza na kuhifadhi silaha za aina yoyote ile wanazozihitaji na kuzitumia wakati wowote wanapolazimika kujilinda. 

Marekani tayari imeshaiwekea vikwazo kadhaa Iran kwa hoja kwamba majaribio yake ya makombora yanakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa. 

Iran hata hivyo inakana kwa kusema haina azma ya kutengeneza makombora ya silaha za kinyuklia.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.