}

Ndege ya Urusi iliyopotea imepatikana Baharini.

Ndege ya Urusi  iliyopotea na mabaki yake kupatikana Baharini.

Norway inasema kuwa kundi la watafutaji limepata mabaki ya ndege ya Urusi aina ya helikopta, ambayo ilianguka baharini ikiwa na watu 8 ndani yake.

Ndege hiyo ambayo ilikuwa haijulikani iliko tangu Alhamisi, kwa sasa iko chini ya bahari karibu na eneo la Barentsburg, kwa mujibu wa maafisa.
Polisi nchini Norway sasa wanaweza kuwatafuta wale waliokuwa ndani ya ndege hiyo, taarifa hiyo ilisema.

Ofisi ya Urusi huko Barentsburg inasema kuwa wahudumu watano na wanasayansi watatu, walikuwa ndani ya ndege hiyo wote raia wa Urusi na kuna hofu kuwa wamefariki.

Ilikuwa katika safari fupi kutoka Pyramiden kwenda Barentsburg eneo la madini la Urusi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.