}

TIKETI ZA KUONA PAMBANO LA SIMBA NA YANGA KUUZWA MWISHO IJUMAA

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limetangaza kuanza kwa uuzwaji wa tiketi za pambano la watani wa jadi Simba na Yanga ,

Pambano la watani hao ambalo linalotarajiwa kuchezwa agost 28 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam tiketi zake zimeanza kuuzwa hii leo na mwisho wa uuzwaji wa tiketi hizo utakuwa siku ya ijumaa.

Alfred Lucas  ambaye ni 
Afisa Habari wa TFF,amesema tiketi hizo zimeanza kuuzwa kuanzia leo hii kwa njia ya mtandao ambapo kiingilio cha chini ni shilingi elfu 10,000 huku kiingilio cha juu kikiwa elfu 20,000

Lucas alisema tiketi hizo zitauzwa hadi siku ya ijumaa ya tarehe 28,siku moja kabla ya mchezo na hakutakua na mauzo ya tiketi siku yenyewe ya mchezo huo hapo jumamosi.

'Ni vyema mashabiki na wadau wa soka wakanunua mapema tiketi hizo ili kuondoa usumbufu ambao huenda ukajitokeza' alisema lucas 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.