}

STARS ITAKAYOIVAA BENINI HII HAPA

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Salumu Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji ishirini na nne ambacho kinatarajia kuingia kambini Tarehe tano mwezi wa kumi na moja mwaka huu kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kalenda ya Fifa dhidi ya benin mchezo utakao pigwa tarehe 11 mwezi ujao.

Wachezaji ambao kocha Mayanga amewaita ni

GOLIKIPA,  Aishi Manula, Peter Manyika na  Ramadhani Kabwili

MABEKI . Boniphace Maganga,  Abdi Banda, Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Nurdin Chona, Erasto Nyoni, na Dickson Job

VIUNGO NI.  Himid Mao, Hamis Abdalah, Mzamiru Yassin, Raphael Daud, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Ibrahim Ajibu, Mohamed Issa, Farid Mussa na Abdul Mohamed

WASHAMBULIAJI . Mbwana Samata, Mbaraka Yusuph, Elias Maguli, na Yohana Mkomola.

Aidha Mayanga alisema  mchezo huo watakaocheza ugenini utakua na tija kubwa kwa timu ya Taifa hasa katika harakati za timu hiyo kujiandaa na michuano ya kufuzu kwa fainali za Afrika.


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.