}

Ocean Road yataadharisha kuhusu athari za Saratani kiuchumi.


Vifo vitokanavyo na saratani ya matiti vinategemewa kuongezeka na kufikia milioni 24 ifikapo mwaka 2035 kama juhudi za kuzuia na tiba hazitaimarishwa katika nchi zenye uchumi wa kati na nchi zinazoendelea kama Tanzania ambapo takwimu zinaonesha kuwa ongezeko la wagonjwa wapya milioni 14.1  hugundulika kila mwaka  na wagonjwa 8.8 hufarikiduni kutokana na ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Julius Mwaiselage amesema athari za kiuchumi zitokanazo na ugonjwa wa saratani ni kubwa na zinaongezeka kila mwaka ambapo mwaka 2010 zimekadiliwa kufikia dola za kimarekani trilioni 1.16 kila mwaka.

Dkt  Mwaiselage amesema takwimu zinaonesha saratani ya matiti inaongoza kuwa na wagonjwa wapya milioni 1.7 kila mwaka ikilinganishwa na wagonjwa laki 5 wanaogundulika na saratani ya shingo ya kizazi. 
Aidha taasisi ya saratani ya ocean road kwa kushirikiana na hoteli ya Kunduchi beach na Hospitali ya Agha Khan wameandaa matembezi ya hisani yatakayofanyika kesho  Oktoba 28 2017 na kuhudhuriwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Mh.Ummy Mwalimu ambayo yana lengo la kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu saratani ya matiti.

Kutokana na kuongeza kwa kasi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo ugonjwa wa kisukari elimu ya zaidi inahitajika kwa watoto ili kuwawezesha kujiepusha na magonjwa hayoa

Hayo yamesemwa na mratibu wa muungano wa vyama vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza Bi.Happy Nchimbi wakati akiwa katika zoezi la upimaji katika shule ya sekondari Jangwani jiji Dar es salaam ambapo amesema ni vyema watu wapewe elimu ya viashiria vya magonjwa hayo mapema ili waweze kujikinga.

Bi.Nchimbi ameongeza kuwa zoezi hili linaenda sambamba na maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa kisukari duniani ambapo wamelenga kutoa elimu hiyo hasa kwa watoto wa kike.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.