}

Idadi ya waliopiga kura nchini Kenya bado ni utata.

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC Wafula Chebukati.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati anaonekana kutoa taarifa za kukinzana kuhusu idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura.
Awali, alikuwa ametangaza kuwa wanakadiria asilimia 48 ya watu waliojiandikisha kupiga kura walijitokeza.
Lakini kwenye Twitter sasa ameonekana kukiri kwamba makadirio hayo yalikuwa ya juu mno.u
Anasema idadi halisi ya wapiga kura waliojitokeza, ambayo wamebainisha kwa sasa, ni wapiga kura 6,553,858.
Tamko la Bw Chebukati sasa linaonesha waliojitokeza kati ya jumla ya 19,611,423 waliojiandikisha kupuiga kura ni asilimia 33.4.
Katika uchaguzi wa tarehe 8 Agosti, waliojitokeza walikuwa 15,073,662 ambao ni sawa na asilimia 78.91.

Chanzo-BBC

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.