}

Azam Fc yatoa angalizo kwa waamuzi ligi kuu.

Na. Anaseli Macha.


Uongozi wa klabu ya azam kupitia kwa msemaji wa klabu hiyo Jafari Idd Maganga umewataka waamuzi wanaochezesha michezo ya ligi kuu Tanzania Bara kufuata sheria 17 za mchezo wa soka ili kuondokana na lawama ambazo wanatupiwa na baadhi ya viongozi wa vilabu pasipo kujali uwezo wa wachezaji wao katika mchezo wa siku hiyo.

Mganga amesema kuwa kwa sasa waamuzi wanajitahidi sana kufuata sheria lakini bado vilabu vimekuwa vikitoa lawama kwao kwa makosa madogo madogo hivyo ni vyema wao wakaongeza ufanisi wao ili kujiondolea lawama ambazo hawastahili.

"wakati mwingine tunatoa lawama kwa waamuzi wetu lakini hatuaangalii wachezaji wetu wamecheza vipi mapka kupelekea matokeo hayo, ni vyema kwa viongozi kwanza kuangalia wachezji wamecheza katika kiwango gani kabla ya kuwalaumu waamuzi'.alisema Jafari.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.