}

KIUNGO WA AZAM AREJEA KUIUA MBEYA CITY KESHO

Kiungo wa Azam Steven Kingue anatarajiwa kurejea katika mchezo hapo kesho baada ya kukaa nje kwa majuma mawili kutokana na kuwa  majeruhi.

Kiungo huyo wa kimataifa alikosa michezo miwili ya kanda ya ziwa ambapo timu yake ya azam ilichuana na mbao fc ya kule Mwanza na baadae kukipiga na Mwadui  ya Shinyanga ambapo katika michezo yote hiyo Azam ilifanikiwa kuapata alama mbili baada ya kupata sare katika michezo yote.

Jafari Idd magana Afisa habari wa klabu ya Azam amesema kurejea kwa kiungo huyo kutampa nafasi kubwa kocha katika kukipanga kikosi chake kuelekea katika pambano lao dhidi ya Mbeya city ambalo linatarajiwa kupigwa hapo kesho majira ya saa moja jioni.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.