}

AZAM WALETEE TUWAUE

Ligi kuu inatarajiwa kuendelea hapo kesho na wikiendi hii katika viwanja mbalimbali ambapo hapo kesho kutakuwa na mchezo mmoja ambao utahusisha wenyeji Azam watakapowakaribisha wagonga nyundo wa mbeya Mbeya City mchezo utakaopigwa katika uwanja wa azam complex ulipo nje kidogo na jiji la Dar es salaam.

Akizungumza na waandashi wa habari, Afisa habari wa klabu ya Azam Jafari Idd Maganga, amesem kikosi kimeendelea na mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kujiwinda na mchezo huo ambapo wanaamini mwalimu amekiandaa vyema kikosi hicho kwa ajili ya kupata ushindi hapo kesho.

Jafari amesema wachezaji na benchi lote la ufundi linamatumaini makubwa ya kufanya vyema katika mchezo wao wa nyumbani ingawa hawakuwa na matokeo mazuri sana katika michezo yao ya kanda ya ziwa ambapo katika michezo miwili wamefanikiwa kukusanya alama 2 tu.


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.