}

Zitto; Wanasiasa wapo hatarini kupoteza haki yao ya Kikatiba kufanya mikusanyiko.

Kiongozi wa chama cha ACT wazalendo Mh.Zitto Zuberi Kabwe.

Kiongozi wa chama cha ACT wazalenda Mh. Zitto Kabwe amesema wanasiasa wako katika hatari ya kukosa haki yao ya msingi kikatiba ya kufanya mikusanyiko kupitia sheria mpya ya vyama vya siasa ambayo rasimu yake tayari imeshatoka.

Akizunguimza jijini Dar es salaam kwenye mdahalo ulioandaliwa na Taasisi isiyo ya kiseriokali ya Policy Forum ambao umeshirikisha wadau mbalimbali na kujadili haki ya kukusanyika Zitto  amesema mazingira ya uhuru wa kukusanyika yako kihalali kwenye katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Kwa upande wake mwandishi wa kujitegemea Pasco Mayala amewataka wanasiasa kuacha kulalamika na kuchua hatua ambazo zitawasaidia kupata haki zao za msingi za kukusanyika kama ilivyotajwa kwenye katiba ikiwemo kufuata taratibu za kisheria.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.