}

NDANDA YAJICHIMBIA SHIROMBO

kikosi cha ndanda kuchele kimetia kambi huko shirombo ili kujiandaa  kabla ya kwenda kuwavaa wakatamiwa wa kagera sukari siku ya jumapili wikiendi hii.

Afisa habari wa klabu ya ndanda Idrisa Bandari amesema kikosi hicho kinaendelea na mazoezi hapo shirombo na kesho mapema asubuhi anatarajia kwenda kagera kwa ajili ya mchezo huo.

Bandari amesema wanamatumaini makubwa katika mchezo wao wa ugenini kufanya vyema kwani wachezaji wana hali nzuri na wamejiandaa vya kutosha hivyo ni jambo la kusubiri Dakika 90 ziatakapoisha.

Ndanda imesafiri kutoka Mtwara hadi shirombo na kutia kambi hapo na kesho inaanza safari nyingine kuelekea kagera kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu Tazania bara dhidi ya kagera Sugar mchezo utakaopigwa siku ya jumapili katika uwanja wa kaitaba.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.