}

MICHUANO YA FA TANZANIA KUANZA TAREHE 31 MWEZI HUU.

Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Salum Madadi. (Picha kutoka. Maktaba)  

Na.Anaseli Stanley Macha.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Jumatano limepanga ratiba ya Kombe la FA (Azam Sports Federation) ambalo Mabingwa watetezi ni Simba.

TFF limepanga jumla ya timu 91 ambazo zitachuana jumla kutoka timu za Mabingwa wa Mikoa, Daraja la Pili (SDL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na ligi kuu.

akizungumza na wana habari jijini Dar es salaam mkurugenzi wa ufundi wa tff Salum Madadi alisema michuano hiyo kwa mwaka huu  imekuja na maboresho mbalimbali ambapo kutaongezeka mizunguko katika michuano hiyo.

Madadi alisema pia kutakuwa na ogezeko la gawio kwa vilabu sambamba na kila hatua ambayo klabu itakuwa inasogea itaongezewa kiwango kidogo cha fedha 

ameongeza kuwa timu za ligi kuu kwa michuano ya awamu hii zitaanza kucheza katika hatua ya pili.

michuano hiyo kwa sasa kutakuwa na Hatua ya awali ambayo itakutanisha timu sita ambazo zimepatikana katika droo ya kwanza kwa timu 51 ambapo inapelekea kupatikana timu 48 ambazo zitaingia katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo.


Mechi za kwanza kwa hatua ya awali za Kombe hilo zinatarajiwa kupigwa Oktoba 31 mwaka huu hadi Novemba 2. ambapo michezo hiyo  itazikutanisha timu za Buseresere (Geita) dhidi ya Green (Songwe), Kisarawe United (Pwani) itacheza na Silabu (Mtwara) na Usamala (Simiyu) wao watapambana na Sahare All Stars (Tanga).



Lakini uzinduzi rasmi wa kombe hilo itakuwa siku ambayo mabingwa, Simba watakapokuwa wanacheza mechi yao ya kwanza.


Upangaji huo wa ratiba ulisimamiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi.



Mchanganuo wa timu hizo ni: 16 za Ligi Kuu, 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL); 24 za Ligi Daraja la Pili (SDL) na 27 za Ligi ya Mabingwa wa Mkoa (RCL).

RATIBA NZIMA HII HAPA

Hatua ya awali;

Buseresere (Geita) vs Green (Songwe), 
Kisarawe United (Pwani) vs Silabu (Mtwara) 
Usamala (Simiyu) vs Sahare All Stars (Tanga).

Hatua ya kwanza
Mashujaa (kigoma) vs Buseresere (Geita)/Green (Songwe),
 Msange (Tabora) vs Mirambo fc (Tabora)
Bulyahulu (shinyanga) vs Area C (dodoma)
Mji mkuu Dodoma vs nyundo (Kigoma)

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.