}

SERIKALI HAINA UGOMVI NA WAIGIZAJI WA NJE

SERIKALI kupitia wizara ya Habari Sanaa utamaduni na michezo imesema haina ugomvi na waingizaji wa filamu za nchi za nje badala yake wametakiwa kufuata utaratibu kwa mujibu wa sheria za nchi.

Akizungumza na wadau wa filamu katika ukumbi wa mkutano wa wizara hiyo uliyopo uwanja wa taifa waziri wa Habari Sanaa Utamaduni Na Michezo Nape Nnauye amesema hakuna haja ya kuzuia kazi za filamu za nje isipokuwa waingizaji na wasambazaji wa kazi hizo wawe na utaratibu mzuri kwa mujibu wa sheria.

Nape amesema kwamba ataendelea kuilinda sheria zilizopo juu ya uingizwaji wa filamu za nje sambamba na uuzaji za nje na ndani mpaka pale itakapo badilishwa


Kwa upande wa wadau wa filamu nchini tumezungumza na Single Mtambalike (Rich Rich) ambapo amesema uamuzi uliotangazwa na waziri mwenye dhamana hii leo umewapa faraja na wanaamini muda wa kula matunda yao umefika.



Naye Jacob Steven (JB) amezungumzia uamuzi huo wa serikali kupitia wizara yenye dhamana na kazi za sanaa, huku akiikumbusha Serikali kuwa bega kwa bega na wasanii ambao wanategemea kazi zao kuendesha maisha.


  

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.