}

ZANZIBAR WATAKA KOMBE LA MUUNGANO KUKUZA SOKA LAO




Mchezaji wa zamani wa timu ya KMKM ya Zanzibar,Abdalah Maulidi amesema kwamba kukosekana kwa michuano ya kombe la Muungano kumesababisha kudhohofisha soka la Zanzibar.

Maulidi amesema kwamba pasipo kuwepo kwa mashindano hayo ya muungano ambayo awali yalikuwa yanazihusisha timu za Tanzania bara na Zanzibar soka la visiwani humo litaendelea kudidimia kwani timu nyingi za huko huwa hazifanyi maandalizi ya kutosha.

Amesema kwamba hata timu ambazo zimepata nafasi ya kuiwakilisha Zanzibar kwenye michuano ya kimataifa,nafasi yao ya kufanya vizuri haipo kwani dalili zimeanza kuonekana katika ushiriki wao wa michuano ya kombe la Mapinduzi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.