}

MARSH KUWAVAA SISTER KESHO



Uongozi Wa Marsh Athetes Academy Kupitia Mwenyekiti Wa Mashindano..Ndg FEYSAL JUMA(snake fey) inawaomba wadau na wapenzi wa soka jijini mwanza na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Ccm kirumba hapo kesho Alhamis ya tarehe 19/01/2017..ili kuipa chagizo timu ya marsh athletes ikipambana na timu ya Sisters toka mkoa wa kigoma katika mchezo wa ligi kuu soka wanawake,,

kundi B..Itakumbukwa kwenye kundi hilo Sisters inaongoza ikifuatiwa na marsh..Sisters ikicheza michezo sita ikishinda yote.haijatoka sare wala kupoteza mchezo..nyavu zake sikiguswa mara moja..

Marsh ikicheza michezo saba ikishinda michezo minne..ikienda sare michezo miwili,, ikipoteza mchezo mmoja kwa kufungwa na Sisters bao mbili kwa bila..

bila shaka mmeona ubora wa hizi timu..ndio maana tunaomba mje kuipa chagizo timu yenu ili mshuudie ikiifunga timu hiyo na kuwa timu ya kwanza kuifunga Sisters...Niimani yetu mtaitikia wito na kufika kwa wingi hapo kesho..

kiingilio ni sh 1000..mwenye uwezo si vibaya akatoa zaid ya hiyo.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na mawasiliano Marsh Athletes Academy

Tarehe 18/01/2017

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.