}

AZAM LIGI KUU YA TANZNIA BARA SIO YA MCHEZO MCHEZO




KLABU BIngwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC,   jana usiku  imelazimishwa sare ya bila kufungana na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Sare hiyo inaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 31 na kubakia nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, ikizidiwa pointi 14 na kinara Simba mwenye pointi 45, ambayo nayo imelazimishwa suluhu na Mtibwa Sugar jana jioni ya leo.

Azam FC iliuanza mchezo huo kwa kasi ikitka kupata bao la mapema, lakini safu ya ulinzi ya Mbeya City ilikuwa imara kuondoa hatari zote zilizokuwa zikifanywa na washambuliaji nahodha John Bocco na Yahaya Mohammed.

Kona iliyochongwa dakika ya 17 na beki Gadiel Michael kuelekea langoni mwa Mbeya City, almanusura izae bao la uongozi kwa Azam FC baada ya mabeki kuiokoa vibaya lakini shuti lililopigwa na Bocco, lilipaa juu ya lango.

Dakika 10 baadaye Yahaya aliwatoka mabeki wawili wa Mbeya City na kuingia ndani ya eneo la hatari lakini alishindwa kumalizia vema kwa kuweka mpira nyavuni baada ya kupiga shuti lililopaa juu ya lango.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilienda kupumzika zikiwa nguvu sawa, kipindi cha pili Azam FC ilijaribu kuimarisha nguvu kwenye eneo la kiungo na ushambuliaji ili kupata bao kwa kuwaingiza Frank Domayo, Samuel Afful na Shabaan Idd kwa nyakati tofauti na kutoka Himid Mao, Yahaya na Joseph Mahundi.

Mabadiliko hayo yaliweza kuiongezea nguvu Azam FC, lakini tatizo kubwa lilionekana kwenye umaliziaji wa nafasi kadhaa zilizotengenezwa huku pia wapinzani wao wakionekana kutafuta sare baada ya kutumia kipindi hicho kupoteza muda,

Jambo jingine kubwa lililoonekana kushangaza watu wengi hadi wachezaji uwanjani, ni maamuzi mabovu katika kipindi cha pili yaliyokuwa yakifanywa na waamuzi kana kwamba wakitaka mtanange huo uishe kwa sare, mwamuzi wa kati Florentina Zabron, mwamuzi msaidizi namba moja Josephat Bulali na namba mbili, Gasper Ketto.

Mwamuzi Florentina, alishindwa kulifanyia uamuzi tukio la kufanyiwa madhambi ya makusudi mshambuliaji wa Azam FC, Shaaban Idd na beki Haruna Shamte wakati akimiliki mpira ndani ya eneo la hatari kuelekea langoni mwa Mbeya City.

Licha ya dakika nyingi kupotezwa kwa mbinu za upotezaji muda za wachezaji wa Mbeya City katika vipindi vyote, mwamuzi wa akiba Omary Kambangwa alionyesha dakika nne tu za nyongeza.

Katika mchezo huo Azam FC iliandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza Tanzania kutumia ubao wa kielektroniki wa kubadilishia wachezaji.


Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Himid Mao/Domayo dk 59, Salum Abubakar, John Bocco (C), Yahaya Mohammed/Afful dk 74, Joseph Mahundi/Shaaban  

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.