}

MAANDALIZI MAZURI YATAIPELEKA STARS AFCON 2019



Kocha wa timu ya vijana ya Tanzania walio na umri chini ya miaka 15,Osca Mirambo Mirambo amesema kwamba Tanzania inaweza kufanikiwa kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2019 endapo kutakuwa na maandalizi ya kutosha kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.

Mirambo amesema kwamba ingawa wadau wa soka baadhi yao wanalizarau kundi letu kutokana na baadhi ya timu kuonekana dhaifu,lakini hicho si kigezo cha kufuzu kwani pasipo kuwa na maandalizi mazuri nafasi ya kufuzu itakuwa finyu.

Timu ya soka ya mipira wa miguu ya tanzania Taifa Stars imepangwa katika kundi moja na timu ya Uganda, Lesotho, na Cape Verde

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.