}

WANAIRINGA WAPIGA MIKAKATI KUIPANDISHA LIPULI




Mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Iringa Spian Kwihava,amesema kwa sasa hakuna mpango wowote ambao unalenga kuipandisha timu ya Lipuli kwa kutumia mbinu mbalimbali ambazo si za kimichezo.

Kwihava amesema kwamba anashangaa kuona kuna baadhi ya wadau wa mpira wa miguu wanadiriki kusema kwamba Lipuli inasaidiwa na baadhi ya viongozi wa TFF ili ifanikiwe kupanda daraja na msimu ujao ionekane katika ligi kuu ya Tanzania bara.

"Hakuna MTU yeyeto kutoka Tff ambaye anatoa msaada wa juu ya jitihada za kuipandisha lipuli, kufanya vizuri kwa timu ya lipuli inatokana maaandalizi mazuri ambayo tmakuwa tukiyafanya hivyo lipuli inafanya vizuri kutokana na sisi wenyewe"alisema kwihava

"Mikakati ambayo tuliyonayo sisi kama wanairinga ndio jukumu tulilolibeba kuhakikisha lipuli inapanda ligi kuu maana lipuli itapandishwa na wanairinga wenyew walio ndani ya iringa na ambao wako nje,tumejipanga na tutahakikisha tunafanikisha adhma yetu "

Kuhusu kutumia hosteli za Tff wakija kucheza dar es salaam Kwihava amesema kwamba wao wanalipia na hawakai bure na isionekana kana kwamba wanapata msaada wanapofikia pale katika hosteli za Tff zilizopo karume jijini Dar es salaam


No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.