}

Waliokosa Pambano la Simba na Yanga kisa uwanja kujaa kurudishiwa Pesa zao.

Na. Anaseli Stanley Macha. 


Kamati maalum ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, imetoa ufafanuzi kuhusu mashabiki wa soka ambao walishindwa kuingia katika uwanja wa Amaan wakati wa mchezo wa hatua ya nusu fainali kati ya Simba dhidi ya Young Africans, wakati mashabiki hao tayari walikua wamekata tiketi za kuingilia ndani ya uwanja na kukosa sehemu za kukaa.
Mjumbe wa kamati  ya mapinduzi cup pia akiwa ni makamo wa raisi wa ZFA taifa kwa upande wa PEMBA, Ally Mohd amesema kamati yake ikishirikiana na wajumbe wezake watawalipa mashabiki hao ili waridhike,ambapo kila shabiki anatakiwa awe na tiketi yake halali.

Aidha Ally Modh amesema wameiona changamoto ya kuchezesha mchezo wa nusu fainali kwa siku moja na katika uwanja mmoja na sasa wataifanyia kazi katika michuano ijayo ili kuhakikisha inakuwa bor na tatizo la kuwakosesha watu waliolip[ia mchezo kushindwa kuona mchezo huo yatakwisha katika michuano hiyo.

hapo kesho michuano hiyo inatarajiwa kufikia tamati kwa mchezo wa fainali kupigwa katika uwanja wa amani visiwani zanzibar ambapo Azam fc watawakaribisha wekundu wa msimbazi Simba. 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.