}

Azam Fc yaitumia Salamu Simba kuelekea mchezo wa kesho.


Kaimu kocha mkuu wa klabu ya Azam FC,Idd Cheche amesema kwamba kikosi chake kimejipanga vyema kuwakabili Simba hapo kesho katika mchezo fainali ya michuano ya kombe la mapinduzi inayofanyika kwenye uwanja wa Amani visiwani Zanzibar.
 
Cheche amesema kwamba wachezaji wake wapokatika hali nzuri na hakuna aliye na majeraha na wote wana morali ya hali juu kuelekea kwenye pambano hilo ambalo linataraji kuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa pande zote.

aidha kocha huyo amesema kwamba mpango wao katika mchezo wa kesho ni kuonesha soka la kiufundi na la kimataifa ambalo kila mmoja atafurahia uwezo watakao uonesha samaba na kurejea chamazi wakiwa na kikombe hicho cha mapinduzi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.