}

Mwambusi wa Yanga akubali kipigo cha Simba, awatupia lawama Wachezaji.


Baada ya kupokea kipigo kikali kwa mikwaju ya Penati kutoka kwa wekundu wa msimbazi Simba,  Kocha msaidizi wa Yanga,Juma Mwambusi amekubaliana na matokeo hayo ya kufungwa licha ya kusema kwamba kikosi chake ndicho kimecheza vizuri tofauti na wapinzani wao katika mchezo huo.

Mwambusi amesema kwamba Yanga ilicheza vizuri kwenye dakika 90 na wachezaji wake wangekuwa makini wangefanikiwa kupata ushindi mapema.

Kwaupande wake kocha msaidizi wa timu ya soka ya Simba,Jackson Mayanja amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kupambana kuhakikisha wanatinga kwenye hatua ya fainali ya michuano ya kombe la mapinduzi.

Mayanja ameyasema hayo kufuatia Simba kuibuka na ushindi kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-2 mbele ya Yanga baada ya dakika 90 timu hizo kushindwa kufungana.

Amesema kwamba mipango yao ilikuwa ni kuingia fainali hivyo matokeo hayo ambayo wameyapata ni mazuri kwao na kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Azam Fc.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.