}

EWURA wapingana na Tanesco kuhusu bei ya Umeme.


Mamlaka ya uthibiti wa mafuta, nishati na maji,-EWURA, imependekeza bei ya umeme kwa watumiaji wote wa umeme unaozidi uniti sabini na tano kuanzia Januari mwakani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Bw.Felix Ngalamgosi amesema kuwa, ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa gharama za  uendeshaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini,-TANESCO.

Ameongeza kuwa, baada ya EWURA kupata maombi ya TANESCO ya kutaka gharama za umeme kupanda kwa asilimia kumi na nane nukta moja tisa na kuwashirikisha wadau, wamefikia uamuzi wa umeme kupanda kwa asilimia nane nukta tano.

Akichanganua kuhusu bei hizo mpya, Bw.Ngalamgosi ameeleza kuwa, umeme kwa wananchi wa kipato cha chini usiozidi unit sabini na tano hautapanda ambapo wateja wa matumizi ya biashara ndogo na taa za barabarani umepanda kwa asilimia saba, mabango na minara asilimia nane.

Hata hivyo, ameitaka TANESCO kuhakikisha kuwa wanazalisha umeme kwa kutumia mitambo ya gharama nafuu na ifikapo Desemba 2017 wawe wamekusanya asilimia tisini na tano ya madeni kutoka kwa wateja wake kusaidia gharama za uendeshaji.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.