}

TFF wakitimiza mikakati yao hii, naliona mbali soka la Bongo.


1.       Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars)

Mwaka huu Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars)  imepata mafanikio makubwa sana kwa kushinda ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Women Challenge). Kuhakikisha kuwa Tanzania inafuzu kucheza fainali za Afrika 2018 na za Dunia 2019.

2.       Serengeti Boys

Hadi sasa timu hii imesafiri na kuweka kambi nchi kadhaa duniani zikiwemo Madagascar,Seychelles,Rwanda ,India na Korea ya Kusini. Hadi sasa kikosi hiki kimecheza mechi 12 za Kimataifa dhidi ya timu kubwa za Taifa ikiwemo ya Marekani,South Korea na Afrika Kusini na kimefanikiwa kushinda mechi saba,sare tatu na kufungwa mechi mbili tu.

Kikosi hiki kinalelewa ili 2019 kifaulu kucheza fainali za Afrika U20 (Afcon U20).

3.       Fainali za Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2019

Tanzania imepewa fursa na Shirikisho la mpira barani Afrika CAF ya kuwa wenyeji wa fainali za Afrika kwa vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019 (Afcon U17).

Hii ni heshima kubwa sana kwa Tanzania na itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kupata uenyeji huu tangia tupate uhuru.

Fursa hii tukiitumia vyema itatupatia mwanya mzuri wa kunyakua ubingwa wa Afrika tukiwa wenyeji wa michuano.

3.1   Fainali za Olimpiki mwaka 2020 Tokyo.

TFF imejizatiti kuhakikisha Timu yetu ya Taifa umri chini ya miaka 23 (Kilimanjaro Warriors) inafaulu kucheza fainali za Olimpiki Tokyo mwaka 2020.

Tanzania haijawahi kufuzu  kucheza mpira wa miguu  katika fainali za Olimpiki. Safari hii tumedhamiria kufuzu.

3.2 Kuelekea kombe la dunia 2026

Matumaini ya TFF ni kuwa muunganiko wa wachezaji bora kutokana na Fainali za Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2019, Serengeti Boys ya sasa na Kilimanjaro Warriors (Timu ya Olimpiki) itakayoundwa Januari mwakani 2017 yatalipatia Taifa letu fursa ya kuunda kikosi imara cha timu ya Taifa (Taifa stars).

Kikosi kitaanza kuonyesha makali yake Afrika na duniani kuanzia mwaka 2021 na kuelekea fainali za kombe la dunia mwaka 2026.

​USHAURI KWA WATANZANIA WENZETU​

1.       Wanaogombea uchaguzi mwakani, wasiyavuruge malengo haya ambayo uongozi wa sasa tayari umeshayapata na kuliletea sifa nyingi Taifa letu.

Tanzania sio kichwa cha mwenda wazimu tena. Serengeti Boys imeonesha njia.

2.       Wahusika wanaotafuta nafasi za uongozi, msiitumie staili iliyotumiwa dhidi ya Mh Aden Rage. Madhara ya staili hiyo na athali zake kwa Taifa ni kubwa na za muda mrefu.

Tujikinge dhidi ya “ultra vires”, kwa masuala ya michezo na hasa soka. Tulenge katika kushindana katika “performance” kwa kufuata sheria zinazotawala sekta ya michezo nchini na duniani.

#Tanzania4tokyo2020

Kwani sisi ni nani tushindwe kushiriki kombe la Dunia 2026? Chonde chonde wapiga kampeni , ambao tayari hila zao zinajulikana, msitumie mbinu chafu kama zilizotumika dhidi ya Mh Rage ili kujenga uhalali.

Tuangalie maslahi mapana ya Taifa kuliko maslahi binafsi ya kusaka Uongozi. Hongera sana Waziri Nape na TFF. Tanzania inasonga mbele kisoka na 2020 kuna mafanikio makubwa ya kucheza soka katika michezo ya Olimpiki tangu Tanzania ipate uhuru.  Hatutaki ujinga.

#Tanzaniasoccer4tokyo2020

​SOKA LA TANZANIA LAPANIA OLIMPIKI TOKYO 2020 NA KOMBE LA DUNIA 2026​

​Kwa kipindi kirefu Tanzania hatujafanikiwa kucheza fainali kubwa za mpira barani Afrika.​

Mara ya mwisho kupata mafanikio makubwa kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) ilikuwa ni mwaka 1980 Tanzania ilipofuzu kucheza fainali za Afrika (AFCON) nchini Nigeria.

Ila kuhakikisha Tanzania inang’ara tena kimataifa katika mpira wa miguu Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) lina nia  ya kuhakikisha Tanzania inafuzu kucheza fainali za kombe la dunia  mwaka 2026

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.