}

MBUNGE KILOMBERO AHUKUMIWA KIFUNGO MIEZI SITA JELA

  


Mahakama ya wilaya ya Kilombero imemuhukumu Mbunge Wa jimbo la Kilombero Mhe. Peter Lijualikali (30) kutumikia kifungo cha miezi sita jela bila faini  kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

Mbunge huyo, akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na mwenzie Stephano Mgata (35) walitenda kosa hilo Machi 1, 2016 saa 4 asubuhi Kwenye kikao cha Baraza la Madiwani katika eneo la Kibaoni ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro 

Pamoja na kuwepo kwa maneno mbalimbali juu ya hukumu hiyo ya kuwa mbunge huyo hataendelea na wadhifa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan amewaeleza wananchi kuwa  hukumu hiyo Mhe. Lijualikali haitamfanya aachie wadhifa wake

"Mbunge Mh. Peter Lijualikali ataendelea na wadhifa wake kwa kuwa sheria inasema ili kupoteza kiti ni lazima uwe umepewa adhabu ya kifungo cha ZAIDI ya miezi sita jela", alisema Kailima

"Ibara ya 67(2)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza mambo yanayotoa sifa ya kuwa Mbunge kutoka  madarakani ni kifungo cha zaidi ya miezi sita jela. Huyu bwana kafungwa miezi sita kwa hiyo bado hajapoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge akiwa gerezani na baada ya kumaliza kifungo chake", ameongeza Bw. Kailima.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.