}

Waziri mkuu Majaliwa asema haya katika sherehe za Maulid

Na. Anaseli Stanley Macha. 
Waziri mkuu Kasim Majaliwa

Waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kuwatumikia Watanzania wote bila kujali imani na dini zao.
Akizungumza katika sherehe za kitaifa za Maulid mkoani Singida Mh.Majaliwa amesema kuna matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza katika jamii na katika kuyachukulia hatua za kisheria Serikali haitabagua mtu kutokana na imani yake ya kidini.
Mh. Majaliwa amesema Serikali iko macho kupambana na tukio lolote lenye nia ya kupoteza amani ya nchi na  kuwataka Watanzania kushirikiana na kutoa taarifa juu ya watu waovu ili hatua zichukuliwe.
Kwaupande wake Mufti Mkuu wa Tanzania,Sheikh Abubakar Zubeiry amewataka waislamu wote kupendana, kuacha majungu,fitna na kuacha kila kitu kisicho na faida.
  
Wakati huohuo serikali imetambua mchango mkubwa wa mashirika ya dini hapa nchini kwa kuimarisha umoja, upendo na ushirikiano kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na waziri wanchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa Umma na utawala bora Mh. Angella Kairuki alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 33 wa dayosisi ya mashariki na pwani uliofanyika wilayani kisarawe mkoani Pwani.

Mh. Kairuki amesema serikali inatambua umuhimu na machangoa mkubwa wa mashirika ya dini katika kuunga mkono jitihada mbalimali za maendeleo kwa wananchi.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.