}

Simba U-20 mabigwa michuano ya vijana ligi yaTaifa.

Na .Anaseli Stanley Macha.


Klabu ya simba imeendelea kuandika historia mpya baada ya kutwaa ubigwa wa michuano ya vijana chini ya miaka 20 ambayo kwa Mara ya kwanza imeanzishwa hapa nchini na shirikisho LA Soka Tanzania .

Simba U20 jana imefanikiwa kuwafunga azam kwa mikwaju ya penati baada ya kwnda sare ya mabao 2  2   katika mchezo wa fainali ambao umepigwa katika majira ya Saa moja usiku katika uwanja wa azam complex chamazi jijini dar es salaam

Klabu ya simba imekuwa na historia ya kuanza kutwaa makombe yote ambayo yanaanzishwa kwa mara ya kwanza  ndani ya Tanzania Na kwa kutwaa kikombe cha michuano ya vijana U20 imedhihirisha kuwa ndiyo timu bora katika Michuano yote ya soka ambayo inaanzishwa.

Uongozi wa simba umeweka bayana kuwa ubora wa vijana wao in kwamba waliandaliw kwa muda mrefu pamoja na kusisitizwa kucheza kwa juhudi kubwa jambo ambalo limewafanikisha kuweza kusawazisha baada ya kutanguliwa kwa mabao 2 1 na kusawazisha na hatimaye kuwa mabigwa wapya wa michuano hiyo.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.