}

Hii hapa mbinu ya serikali katika kutokomeza Ukatili.

Na Anaseli Stanley Macha. 

Mh. Ummy Mwalim. 

Ilikutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, serikali kwa kushirikiana na wadau imekuwa ikichukuwa hatua mbalimbal ikiwemo kuanzisha na kuzijengea uwezo timu za ulinz na usalama wa mtoto katika ngazi mbalimbali za mamlaka za serikali za mtaa.

Hayo yamesemwa na waziri wa afya maendeleo ya jamii wazee na watoto Mh.UMMY A.MWALIMU wakat akizindua mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto 2017/18 hadi 2021/22 uliofanyika jijin Dar es salaam.

Aidha Mh.Ummy ameelezea kuwa bado kuna changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiathiri jitihada za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwemo huduma zisizotosheleza kwa waathirika wa vitendo vya ukatili na imani potofu kuhusu matumizi ya huduma zilizopo.

Hata hivyo Mh.Ummy ameongezea kuwa Tanzania ni moja ya nchi nne Dunian zenye mpango wa aina hii unaolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto hivyo nijukumu letu sote. 

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.