}

Usajili mbeya city bado siri.

Na. Geofrey Donatus Jacka. 


Uongozi wa timu ya soka ya Mbeya City umesema kwamba hadi kufikia sasa bado hakuna taarifa rasmi juu ya swala zima la usajili wa dirisha dogo na maswala mengine yanayohusiana na klabu hiyo.
 
Afsa Habari wa timu hiyo Dismas Teni amesema kwamba kwa sasa uongozi unasubiri taarifa kutoka kwa kocha mkuu ili kuwafahamisha mashabiki wa timu hiyo.
 
Amesema kwamba hata swala la mchezaji Joseph Mahundi litazungumzwa baada ya taarifa ya kocha mkuu ingawa mchezaji huyo tayari ameshaonekana katika klabu ya Azam.

Kikosi cha timu ya vijana walio na umri chini ya miaka 15 kinaendelea vyema na program mbalimbali huko visiwani Zanzibar ambapo timu hiyo inacheza michezo mbalimbali ya kirafiki kwa ajili ya kupata timu bora itakayocheza fainali za vijana zitakazofanyika hapa nchini mwaka 2019.
 
Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba timu hiyo jana ilicheza mchezo wa kirafiki na Zanzibar kombaini na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 8-1.
 
Lucas amesema kwamba dhumuni kubwa la michezo hiyo ni kuongeza wachezaji wenye vipaji kwa ajili ya kuungana na wenzao ili kujiandaa na michuano hiyo ya Afrika kwa vijana ambayo Tanzania itakuwa mwenyeji wa fainali hizo.

No comments

Haki zimehifadhiwa. Copyright, kituochahabari.com ©2016. Blog designed by Geofrey Donatus Jacka.. Powered by Blogger.